Mpiga picha wa Atabatu Abbasiyya tukufu amekuwa mshindi wa kwanza kwenye mashindano ya kimataifa

Maoni katika picha
Mpigapicha Liith Musawi mtumishi wa kituo cha uzalishaji wa vipindi na upigaji picha Alkafeel chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, amepata nafasi ya kwanza katika mashindano ya kimataifa (Hubbu Almuharram) awamu ya sita, yaliyo simamiwa na wizara ya utamaduni na habari ya Iran, jumla ya wapigapicha (1480) wameshiriki kutoka kwenye nchi ishirini, na jumla ya kazi (10230) zimeshindanishwa.

Liith Musawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hili ni miongoni mwa mashindano muhimu ya kimataifa, ambalo wapiga picha wengi kutoka nchi tofauti hushiriki kila mwaka, mimi nimeshiriki kwa kutuma picha iliyobeba jina la (Hussein ni meli ya uokovu), hakika ushindani ulikuwa mkubwa, nimebahatika kuwa mshindi wa kwanza”.

Akaongeza kuwa: “Picha niliyopiga niliipamba kitaalam kushinda picha zote nilizowahi kupiga, picha hiyo ilionyesha malalo mbili takatifu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) majira ya jioni, ilikuwa na mazingira mazuri yanayo endana na malalo hizo.

Kumbuka kuwa kushiriki kwenye mashindano haya na kupata ushindi ni moja ya mfululizo wa ushindi wanaopata wapiga picha wa Atabatu Abbasiyya tukufu, katika mashindano ya kitaifa na kimataifa, kutokana na ujuzi walionao pamoja na ushirikiano mkubwa wanaopewa na Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo hufanya kila iwezalo katika kuendeleza viwango vya watumishi wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: