Kukamilika kwa utengenezaji wa umbo la dirisha la mbao la bibi Zainabu (a.s)

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha kutengeneza madirisha na milango ya makaburi matukufu na mazaru chini ya Atabatu Abbasiyya, wamemaliza kutengeneza umbo la mbao la dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s), sambamba na kuendelea na utengenezaji wa sehemu za madini ya dirisha hilo, yatakayo wekwa kipande baada ya kipande.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naadhim Ghurabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika utengenezaji wa dirisha unapitia hatua mbalimbali, kulingana na kila sehemu ya dirisha (madirisha – nguzo za pembeni – sehemu za maandishi ya Quráni na mashairi – sehemu ya juu ya durisha – mapambo - nguzo za dirisha), kazi imepiga hatua kubwa ukilinganisha na ilivyo kadiriwa, ujenzi huo umeenda pamoja na utengenezaji wa vitu vingine”.

Akaongeza kuwa: “Mafundi selemala wamefanya kazi kubwa, wamejenga umbo hilo kwa umaridadi na ustadi mkubwa, wamechagua mbao bora zaidi za (Burma), zinazo endana na uzito zitakao beba”.

Akabainisha kuwa: “Umbo la mbao linasifa nyingi, miongoni mwa sifa zake ni:

  • - Umbo la dirisha limejengwa kwa umbo la mstatili.
  • - Urefu mita 3.70.
  • - Upana mita 4.69.
  • - Urefu wa kimo (chini hadi juu) mita 4.04.
  • - Taji (kofia) inaurefu wa (mt4.15) na upana wa (mt3.15) na urefu wake (mt1.10)”.

Akafafanua kuwa: “Umbo linanguzo nne kuu na nguzo kumi za katikati zinazo tengenisha sehemu za madirisha, chini kuna reli nne zinazo shikilia ngozo kwa chini, zimewekwa madini ya (silva) safi kwa ujazo wa (ml 5), kwa ajili ya kuzipa uimara na kudumu kwa muda mrefu, pamoja na fito nne za juu zinazo shika nduzo kuu, kisha kuna fito zingine zinazo saidia kushika taji (paa) na mapambo pamoja na ufito wa maandishi”.

Kumbuka kuwa mbao zilizo tumika ni aina ya Burma, ni mbao bora na imara zaidi, zinauwezo mkubwa wa kuvumilia mazingira ya baridi na joto, zinaweza kubeba mzigo mzito, haziliwi na wadudu, mbao zimetengenezwa kwa kufuata vipimo vya dirisha, kazi hii imefanywa chini ya usimamizi wa mafundi waliobobea katika fani hiyo, kila kitu kimetengenezwa kwa kufuata vipimo vya kihandisi na kwa ustadi mkubwa. Ubora, uimara na uzuru wa umbo hili unazidi mara nyingi umbo la zamani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: