Kitabu hiki kinatokana na kazi za mhakiki mkubwa Haafidh ibun Asaakir Taqiyu-Dini Abu Qassim Ali bun Hibatu-Llah bun Abdullahi Dimashqi, aliyekufa mwaka 571h.
Kitabu hiki chenye kurasa (158) kimehakikiwa na ustadh Masudi Mahadi Zaadah, chini ya usimamizi wa Shekh Qais Bahjat Atwaar na kikapitiwa na kamati ya wataalam wa kituo hicho, kitabu kinasehemu kuu tatu ambazo ni:
- - Sehemu ya kwanza inaelezea historia ya muandishi.
- - Sehemu ya pili inaelezea utukufu wa Ahlulbait (a.s) katika uandisi wa Haafidh bun Asaakir.
- - Sehemu ya tatu ni utafiti kuhusu uhakiki, baada yake ikafuata milango (16) iliyo hakikiwa.
Mhakiki wa kitabu Ustadh Masudi Mahadi Zaadah akasema: “Pokezi za Haafidh Damashqi katika sifa za kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) hazipatikani kwa wingi katika historia yake, bali kwa kiwango kikubwa zipo katika vitabu vyake vingine na kwenye vikao darasa vyake mbele ya wanafunzi wake na wasikilizaji wake”.
Akaendelea kusema: “Baadhi ya masomo yake, yanaeleza kuhusu utukufu wake, yakiwemo ambayo sisi tunazungumzia, nalo ni juzuu la ishirini na moja baada ya shughuli miambili ishirini na mbili, kuna juzuu mbili maalum zinazo zungumzia utukufu wa Ali bun Abu Twalib (a.s), ambao haujaandikwa na kusambazwa hapo kabla, Mwenyezi Mungu mtukufu ametuwezesha sisi kuandika na kusambaza katika maktaba duniani na kufikisha mbele ya mwanafunzi mtukufu”.
Kumbuka kuwa kituo cha turathi za kiislamu kinahusika na kufanya hakiki za vitabu, makao makuu yake yapo katika mji wa Mash-hadi, nacho ni miongoni mwa vituo muhimu vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu nje ya Iraq.