Multaqal-Qamaru katika ugeni wa mkoa wa Diyala

Maoni katika picha
Kikosi cha kituo cha Multaqal-Qamaru chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimewasili katika mkoa wa Diyala mtaa wa (Jadidatu-Shatu), kwa ajili ya kudumisha mawasiliano kwa vijana, na kuongeza hazina yao kiutamaduni pamoja na kuwawezesha kupambana na changamoto wanazo kutana nazo katika maisha.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa kituo Shekh Harith Dahi aliyotoa kwa mtandao wa Alkafeel, amesema: “Ziara za kitamaduni na utowaji wa maelekezo ni kazi muhimu ya kituo chetu, tunamkakati wa kutembelea mikoa yote ya Iraq, chini ya ratiba maalum, iliyo pitishwa na kupata baraka za uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ambao uko mstari wa mbele kusaidia kila kitu kinacho wezesha kumjenga na kumuendeleza mwanadamu”.

Akaongeza kuwa: “Ziara yetu imehusisha ufanyaji wa vikao na viongozi wa mtaa tajwa, tumekubaliana kuendesha program za kitamaduni katika mkoa huu, aidha tumefanya vikao viwili katika Husseiniyya ya maukibu ya (Mwenye ubavu uliovunjika), mada ya kwanza ilikuwa inasema: (Kuimarisha sekta ya elimu katika maadhimisho ya Husseiniyya kwa mujibu wa maelekezo ya Marjaa Dini mkuu), na mada ya pili imetolewa na Ustadh Hassan Jawadi mmoja wa wahadhiri wa kituo, chini ya anuani isemayo: (Kujenga utambulisho)”.

Washiriki wa nadwa hizo wametoa pongezi nyingi na shukrani za dhati kwa Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa juhudi kubwa wanayo fanya katika kuwatumikia raia wa Iraq wakiwemo watu wa mkoa wa Diyala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: