Maahadi ya Quráni tukufu katika mji wa Najafu imekamilisha maandalizi ya semina ya walimu

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya, imekamilisha maandalizi ya semina ya walimu katika somo la (maarifa ya Quráni), na (Kanuni za tajwidi).

Sayyid Muhandi Almayali amesema kuwa: “Mradi wa Quráni kwa wanafunzi wa Dini, umekamilisha maandalizi ya kupokea wanafunzi wa semina, itakayo fanyika kwa muda wa wiki mbili (saa 6) kwa siku, itaanza siku ya Jumapili (20 Juni 2021m), semina hii inalenga kuandaa walimu wa (maarifa ya Quráni) na (kanuni za tajwidi)”.

Akasema: “Hii ni semina ya kwanza kufanywa kwa mtindo huu hapa Iraq na katika nchi za kiarabu, inalenga kuwawezesha wanafunzi wa hauza kufundisha kwa usahihi Quráni tukufu”.

Tambua kuwa idadi ya wanafunzi watakao shiriki kwenye semina ni zaidi ya (40) kutoka Iraq na baadhi ya nchi za kiislamu.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu kupitia matawi mbalimbali ni moja ya vituo muhimu vya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, inalenga kufundisha elimu za Quráni, na kutengeneza jamii inayofanyia kazi mafundisho ya Quráni na sunna pamoja na uwezo wa kufanya tafiti katika fani tofauti za Quráni tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: