Idara ya mahusiano ya vyuo na shule chini ya ofisi ya mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetoa wito kwa wadau wa elimu mtandao, washiriki kwenye warsha ya kielimu inayo husu (Nafasi ya mawasiliano na simu za kisasa (smartphone) katika kuboresha ufundishaji wa kutumia mitandao hapa Iraq), itakayo fanywa kwa kushirikiana na chuo cha Twafu na kikosi cha mawasiliano kutoka wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu.
Warsha itafanywa chini ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, asubuhi ya Jumanne (22 Juni 2021m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na kurushwa warsha hiyo kwenye mitandao.
Rais wa kitengo hicho Ustadh Muhammad Ali Azhar ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Warsha hii ni muendelezo wa warsha iliyotangulia, kitu cha pekee kwenye awamu hii ni kujadili mada muhimu ya ujifunzaji kwa kutumia mitandao ya mawasiliano ya mashirika ya Iraq, kwani mashirika hayo ndio nguzo kuu za kukuza ujifunzaji wa kutumia mitandao, watahudhuria kwenye warsha hiyo wadau wafuatao (Mashirika ya mawasiliano – Wizara ya malezi – Wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu), pamoja na wawakilishi kutoka vyuo vikuu vya Iraq na mashirika mengine”.
Akaongeza kuwa: “Tunatarajia warsha hii itaweka msingi imara wa usomaji kwa njia ya mtandao, kwani jambo hilo limekuwa na umuhimu mkubwa kwenye usomaji wa hatua zote, jumla ya mada tisa zitawasilishwa na wasomi bobezi katika fani hiyo, mada zote zinalenga namna bora ya kujifunza kwa kutumia mtandao”.