Mazingira ya furaha yametanda katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Nyoyo zinatembelea Ataba takatifu zikiwa zimebeba ubendo na mauwa ya furaha, jua la uongofu wa Ridhwa limechomoza, dunia imejaa shangwe na furaha, kwa nini furaha isienee wakati kazaliwa mwezi miongoni mwa miezi ya Muhammadiyya, Imamu wa nane Ali bun Mussa Ridhwa (a.s).

Kufuatia kumbukumbu hiyo tukufu, kuta za Atabatu Abbasiyya na korido zake zimewekwa mapambo yanayo ashiria furaha, na kuwekwa vitambaa vyenye ujumbe mzuri, taa za rangi maalum kwa ajili ya matukio ya furaha zimewashwa ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na kuweka mauwa na miti ya mapambo, na maneno mazuri ya pongezi yamewekwa katika milango ya haram tukufu.

Ataba imeandaa ratiba maalum ya kupokea mazuwaru wanaokuja katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kuadhimisha tukio hili tukufu kwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), Ataba imeweka utaratibu maalum wa kuadhimisha tukio hili takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: