Watumishi wa kikosi cha Abbasi wanafanya opresheni kubwa ya kupuliza dawa katika chuo kikuu cha Waasit

Maoni katika picha
Watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Liwaau/26 Hashdu-Shaábi, wanafanya opresheni kubwa ya kupuliza dawa katika chuo kikuu cha Waasit na vitengo vyake pamoja na kumbi za madarasa.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa: Opresheni hii inalenga kupambana na kuenea kwa virusi vya Korona, na kulinda usalama wa walimu na wanafunzi.

Akaongeza kuwa: Kikosi chenye mafunzo maalum ya kutumia vifaa vya kisasa vya kupuliza dawa ya kujikinga na maambukizi kimeendesha program hiyo kwenye majengo ya chuo kikuu na vitengo vyake pamoja na ndani ya kumbi za madarasa.

Uongozi wa chuo umeshukuru sana kikosi cha Abbasi kwa kufanya program hiyo, pamoja na kazi kubwa wanayo fanya ya kupambana na virusi vya Korona tangu lilipo tangazwa tatizo hili kwa mara ya kwanza.

Tambua kuwa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, kimesha fanya shuguli nyingi za kibinaadamu tangu lilipozuka janga la virusi vya Korona, ikiwa ni pamoja na kupuliza dawa za kujikinga na maambukizi kwenye mikoa tofauti na kujenga kituo maalum cha (Yaasin) mjini Karbala, kinacho simamia kuonsha na shughuli za maziko kwa watu waliokufa na ugonjwa wa Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: