Katika ufunguzi wa warsha ya ufundishaji wa njia ya mtandao: Atabatu Abbasiyya imesisitiza kusaidia sekta ya elimu

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu katika hafla ya ufunguzi wa warsha ya ufundishaji wa njia ya mtandao hapa Iraq, iliyofanywa katika Atabatu Abbasiyya imesisitiza kusaidia sekta ya elimu, na daima itaenda na mabadiliko ya nchi, na kuhakikisha inafanya kulingana na mahitaji ya mabadiliko, sawa iwe katika sekta ya maisha au elimu.

Muwakilishi wa Ataba Dokta Muayyad Ghazali ambaye ni rais wa chuo kikuu cha Al-Ameed, katika ujumbe aliowasilisha kwa niaba ya katibu mkuu, amesema kuwa: “Tangu lilipoanza janga la virusi vya Korona na kuathiri sekta ya elimu, Atabatu Abbasiyya imetafuta njia mbadala ya kutoa huduma kulingana na mahitaji ya jamii, upande wa elimu ikaanzisha utaratibu wa elimu masafa (kusoma kwa njia ya mtandao)”.

Akaongeza kuwa: “Taasisi zote za Atabatu Abbasiyya tukufu za malezi na elimu, hazikuacha kutoa huduma wakati wa janga la Korona, ziliendelea kutoa huduma kwa kutumia njia ya mtandao, ambayo imesaidia kulinda sekta ya elimu”.

Akabainisha kuwa: “Taasisi za Atabatu Abbasiyya za kielimu kama vile chuo kikuu cha Al-Ameed na chuo kikuu cha Alkafeel pamoja na kituo cha taaluma Alkafeel, zinafanya warsha ya kielimu kwa kushirikiana na viongozi wa chuo cha Twafu, katika sekta muhimu ambayo ni (nafasi ya mashirika ya mawasiliano na simu ganja katika uboreshaji wa elimu kwa njia ya mtandao), chini ya usaidizi wa wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu”.

Kumbuka kuwa warsha hii iliyopewa jina la (nafasi ya mashirika ya mawasiliano na simu ganja katika uboreshaji wa elimu kwa njia ya mtandao), imefavywa kwa ushirikiano wa wawakilishi wa wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu pamoja na chuo cha Twafu, ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka wizara ya (elimu ya juu na tafiti za kielimu, malezi na mawasiliano), pamoja na ugeni kutoka chuo kikuu cha Al-Ameed.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: