Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya hafla ya wanawake kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s), ndani ya moja ya Sardabu za haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhudhuriwa na mubalighaat na wahadhiri pamoja na mazuwaru.
Makamo kiongozi wa idara hiyo bibi Taghridi Tamimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hafla hii ni sehemu ya harakati za idara katika kuadhimisha matukio ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) kwa kufuata utaratibu maalum kwenye kila tukio, hafla inautaratibu maaluma na idadi ya washiriki kutokana na kuwepo kwa janga la virusi vya Korona”.
Akaongeza kuwa: “Hafla imefunguliwa kwa Quráni tukufu, kisha zikafuata baadhi ya kauli za Imamu Ridhwa (a.s) pamoja na kusherehesha kila kauli yake na kutaja madhumuni ya kauli hiyo, pamoja na kuowanisha na mazingira halisi tunayo pitia kwa sasa, na kuangazia faida inayopatikana”.
Akamaliza kwa kusema: Aidha kaswida, tenzi na mashairi mbalimbali yamesomwa, sambamba na kufanya shindano kuhusu Imamu Ridhwa (a.s), na kugawa zawadi kwa washindi, mwisho ikasomwa dua ya Faraj ya Imamu Mahadi (a.f).