Makumbusho ya Alkafeel inaendesha semina kuhusu njia za kuweka rangi za kienyeji

Maoni katika picha
Makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya inaendesha semina kuhusu uwekaji rangi ya kienyeji kwenye vifaa mbalimbali, kwa watumishi wa idara ya utunzaji na maabara pamoja na idara ya ukarabati na miswala, ili kuongeza uwezo wa watumishi hao.

Rais wa kitengo cha makumbusho Ustadh Swadiq Laazim ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hii ni moja ya semina nyingi wanazopewa watumishi wa makumbusho, kila mmoja anashiriki kwenye semina inayo endana na fani yake, makumbusho inavitu vingi vilivyo tengenezwa kwa mikono, kama vile miswala na vitambaa, vitu hivyo ni vya asili na hupakwa rangi ya asili”.

Akaongeza kuwa: “Mkufunzi wa semina hii ni Ustadh Ahmadi Swagiir naye ni mtaalamu wa fani hiyo, wanafundishwa kwa nadhariyya na vitendo, wamefundishwa mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo ni utengenezaji wa rangi itokanayo na mimea pamoja na kufanya kila rangi iendane na sehemu inapo hitajika, katika somo la vitendo wanafanya kazi halisi kutokana na waliyo fundishwa, tunamshukuru Mwenyezi Mungu matokeo ya kazi zao ni mazuri, nimatumaini yetu kuwa washiriki wameongeza ujuzi kwa kiwango kikubwa”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu huandaa na kusimamia semina na nadwa za fani mbalimbali, ikiwemo semina hii, kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi wake kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: