Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu chini ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ni miongoni mwa vitengo muhimu katika uandishi na uchapishaji wa vitabu.
Rais wa kitengo hicho Mheshimiwa Shekh Ammaar Hilali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tangu kuanzishwa kwa kitengo chetu hadi sasa, tumesha chapisha idadi kubwa ya vitabu na majarida katika mada tofauti, Fiqhi, Adabu, Historia na jamii, vitabu hivyo vinahitaji soko sahihi na dirisha kubwa la kuwafikia wanafunzi na wadau wa elimu, hivyo tunamaonyesho ya kudumu katika uwanja wa katikati ya haram mbili, karibu na Atabatu Abbasiyya tukufu, mkabala na mlango wa Imamu wa zama (a.f)”.
Akaongeza kuwa: “Maonyesho hayo ni sehemu nzuri kwa mtu yeyote anayetaka kuona vitabu vyetu, vimepangwa vizuri na vinaonekana bayana”.
Akasisitiza kuwa: “Maonyesho ya vitabu ya kudumu ni njia maalum ya kuona vitabu vyetu vyote, lengo ni kunufaika kielimu wala sio kipesa, tumekuwa tukiboresha maonyesho hayo kila wakati na kuhakikisha yanaendana na thamani ya elimu inayo onyeshwa, na kuyafanya kuwa na thamani kubwa kwa kila anaye yatembelea”.
Akahitimisha kwa kusema: “Milango ya maonyesho iko wazi kwa kila mtu katika siku zote za wiki, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atupe manufaa zaidi katika uwanja wa elimu na maarifa”.