Kamati ya majaji wa shindano la (Chuo changu mboni yangu) lililoandaliwa na idara ya habari na mahusiano ya vyuo kwa kushirikiana na kitengo cha harakati za wanafunzi katika chuo kikuu Alkafeel, imetangaza majina ya washindi wa shindano hilo.
Rais wa kamati hiyo Dokta Farasi Muhammad Kaamil amesema kuwa: “Shidhano liliandaliwa kwa lengo la kujenga uwezo wa wanafunzi na ushindani baina yao, tumefuata vigezo vyote vya msingi katika kutoa alama”.
Akaongeza kuwa: “Chuo kimeratibu mashindano mengi katika fani tofauti, ili kujenga kizazi cha wanachuo waliokamilika kila upande”.
Akasema kuwa: “Jumla ya wanafunzi (71) kutoka vyuo vikuu tofauti wameshiriki katika shindano hili baada ya kuangalia kazi zao, matokeo yalikua kama ifuatavyo:
Mshindi wa kwanza: Baniin Yunusi Kaamil, kazi yake ilikua na picha (10).
Mshindi wa pili: Zaharaa Salim Abiis, kazi yake ilikua na picha (34).
Mshindi wa tatu: Ammaar Mansuur Rahim, kazi yake ilikua na picha (32)”.