Kituo cha kukarabati nakala-kale hupitia hatua tofauti katika kukarabati nakala-kale adim za kihistoria

Maoni katika picha
Kituo cha ukarabati wa nakala-kale chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya ni miongoni mwa vituo muhimu, kinafanya kazi kubwa ya kukarabati vitabu na nakala-kale adimu na kuvilinda visiharibike kwa kutumia mbinu za kisasa.

Pamoja na kuwa na muda mfupi tangu kuanzishwa kwake, ambapo kwa sasa imefika miaka kumi, kimefanikiwa kukarabati mamia ya nakala-kale na vitabu vilivyo andikwa katika miongo tofauti, pamoja na misahafu mingi baada ya kutelekezwa kwa muda mfefu kabatini na kuharibika, vitabu hivyo sasa vipo katika muonekano mzuri na vimeingia mikononi mwa wasomaji na watafiti.

Kituo kimejaa vifaa vya kisasa vinavyo endana na utaalamu wa watumishi, hakika wanafanya kazi nzuri sana.

Kituo kinavitengo vitano vinavyo fanya kazi kwa ushirikiano kama nyuki ya kukarabati na kurudisha ubora wa nakala-kale, vitengo hivyo ni:

  • - Maabara ya bailojia.
  • - Maabara ya kemia.
  • -
  • - Kazi za kitaalamu na mapambo.
  • - Utunzaji wa nakala-kale.

Kituo kimekuwa sehemu muhimu ya kazi hizi ndani na nje ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: