Maahadi ya Quráni tukufu katika mji wa Najafu inafanya semina ya kuandaa walimu

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu, inafanya semina ya kuandaa walimu wa Quráni na tajwidi, katika mradi wa Quráni kwa wanafunzi wa Dini, washiriki wapo arubaini kutoka ndani na nje ya Iraq.

Wanafundishwa kwa nadhariyya na vitendo chini ya walimu bobezi katika somo la Quráni, pamoja na somo la njia za ufundishaji, wanasoma kwa muda wa saa sita (6) kwa siku.

Semina itafanyika kwa muda wa wiki mbili, kwa lengo la kuwawezesha washiriki kuelewa vizuri masomo watakayo fundishwa, na kupanua wigo wa manufaa.

Tambua kuwa mradi wa Quráni kwa wanafunzi wa masomo ya Dini ni miongoni mwa miradi muhimu katika Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu, unapewa umuhimu mkubwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kwani ni sehemu la lengo lake kuu la kutumikia vizito viwili vitakatifu, mradi huu unafanyika kwa mwaka wa tano mfululizo, tayali mamia ya wanafunzi wa hauza ya Najafu wamesha nufaika nao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: