Kitengo cha miradi ya kihandisi kimesema: Tumejenga vituo (25) vya kusafisha maji na kuwapa wananchi bure

Maoni katika picha
Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimejenga vituo (25) vya kusafisha maji (R.O station), ndani na nje ya mji wa Karbala kwa ajili ya kuwapa wananchi maji masafi, vinauwezo wa kuzalisha zaidi ya lita elfu (80) kwa saa.

Rais wa kitengo hicho Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh amesema: Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya miradi mingi ya utoaji wa huduma, ikiwemo inayogusa maisha ya raia wa Iraq moja kwa moja, imejitahidi kupunguza shida za wananchi kadri ya uwezo wake, miongoni mwa shida kubwa iliyokuwa inasumbua raia wengu ni tatizo la maji safi na salama, ndipo kitengo chetu kikaanza ujenzi wa vituo vya kusafisha maji ndani na nje ya mkoa wa Karbala.

Akaongeza kuwa: Vituo vimejengwa katika miji yenye shida ya maji pamoja na kwenye vituo vya afya na mashambani, kuna kazi za kila siku zinaendelea kwa ajili ya kuhakikisha vituo vinafanya kazi kwa ufanisi, kazi yetu haijaishia kwenye kujenga vituo peke yake, bali kuna kazi zingine tunafanya, kama kujenga vituo vya umeme na zinginezo, kulingana na eneo husika.

Akafafanua kuwa: Kazi ya kujenga vituo vya maji inafanywa na watumishi wa kitengo cha maji, wenye uzowefu mkubwa katika sekta hiyo, baada ya ujenzi na kuanza kazi hukaguliwa na kufanyiwa matengenezo kila wakati kwa ajili ya kuhakikisha huduma haisimami.

Kumbuka kuwa, pamoja na tuliyo sema: kituo kikuu cha kusafisha maji katika Atabatu Abbasiyya kinasambaza maji safi kwa mazuwaru na kwenye majengo yanayotumika kuhudumia mazuwaru, pamoja na maeneo yaliyochini ya Ataba tukufu ndani na nje ya Ataba sambamba na kusambaza maji kwa wakazi wa mji wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: