Chuo kikuu Alkafeel kimekua mwenyeji wa mkutano wa viongozi wa vyuo vya Kiislamu vya Iraq

Maoni katika picha
Chuo kikuu Alkafeel siku ya Jumapili, kimekua mwenyeji wa mkutano wa wakuu wa vyuo vya kiislamu na vitengo vya kiislamu katika vyuo vikuu vya Iraq.

Rais wa wakuu wa vyuo vikuu vya kiislamu vya hapa Iraq Dokta Muhammad Jawadi Twarihi amesema kuwa: “Uongozi wa kamati umepanga kufanya mikutano yake sehemu tofauti za vyuo vya kiislamu vya Iraq, kwa lengo la kuweka mipango ya maendeleo, pamoja na kuandaa mikakati ya kuboresha vyuo vyetu”.

Akaongeza kuwa: “Tulicho pata leo katika chuo kikuu Alkafeel kinaburudisha nyoyo na kutupa matumaini ya kuwa na Iraq bora kielimu, nimatarajio yetu maendeleo haya yaenee kwenye vyuo vikuu vyote vya Iraq”.

Rais wa chuo kikuu cha Alkafeel Dokta Nuuris Dahani amesema kuwa: “Leo chuo kikuu cha Alkafeel kimekua mwenyeji wa mkutano wa wakuu wa vyuo vya kiislamu binafsi na vya serikali, kwa lengo la kuangalia ufundishaji wa vyuo hivyo na kuangalia mifumo ya ufundishaji kwa njia ya mtandao”.

Makamo mkuu wa chuo Dokta Wasam Muhammad Mash-hadani amesema: “Leo tumeshiriki kwenye mkutano huu na kujadili mambo mengi, miongoni mwa tuliyo jadili yanahusu selebasi za masomo, aidha tumeona maendeleo ya kielimu katika chuo kikuu Alkafeel pamoja na vifaa walivyo navyo na mazingira mazuri ya kielimu, tumenufaika na tuliyo ona, tutajitahidi kuyafanyia kazi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: