Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha habari na utamaduni, inazaidi ya aina 250 ya vitabu kwenye maonyesho ya kimataifa yanayo fanyika katika mji wa Kuut awamu ya kwanza, yamezinduliwa siku ya Jumatatu katika ukumbi wa chuo kikuu cha Kuut, yataendelea kwa muda wa wiki mbili.
Maonyesho yanasimamiwa na chuo kikuu cha Kuut kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Waasit, makumi ya taasisi za usambazaji wa vitabu zimeshiriki kwenye maonyesho haya.
Ustadh Muhammad Aáraji kiongozi wa tawi linaloshiriki kwenye maonyesho haya amesema: “Maonyesho yanafanywa kwa mara ya kwanza katika mkoa huu, pia ushiriki wetu ni muendelezo wa ushiriki katika maonyesho ya kimataifa na kitaifa, banda letu limejaa vitabu vya aina tofauti pamoja na vitabu vya mtiririko wa majuzuu (mausua) ikiwemo mausua ya fatwa kifaya ya jihadi ya kujilinga kilicho chapishwa hivi karibuni na Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Akaongeza kuwa: “Ushiriki wetu umetokana na mualiko tuliopewa na kamati ya maandalizi, watu waliohudhuria hafla ya ufunguzi wametembelea banda letu na kuangalia vitabu tulivyo navyo pamoja na kusikiliza maelezo kutoka kwa wasimamizi wa maonyesho haya, wametoa pongezi nyingi, akiwemo rais wa chuo kikuu cha Kuut Dokta Twalib Mussawi, akasema kuwa ushiriki wetu unamchango mkubwa katika maonyesho haya”.
Tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu limepata muitikio mkubwa kutoka kwa watu wanaokuja kutembelea maonyesho, kutokana na kuwa na machapisho yanayokata kiu yao, na yanayo faa kwa watu wa rika zote.