Balozi wa Uturuki: Nilihisi mazingira ya kiroho nilipokua katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Asubuhi ya leo siku ya Jumanne, balozi wa Uturuki nchini Iraq Mheshimiwa Ali Ridhwa Koni na wasaidizi wake, wamefanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), hii ni ziara ya kwanza tangu achukue madaraka hayo.

Baada ya kumaliza ibada ya ziara ametembelea sehemu mbalimbali ndani ya haram takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ameangalia mali-kale zilizopo katika makumbusho ya Alkafeel, na akakutana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar, amemkaribisha na kumuombea mafanikio katika kazi yake, pamoja na kumueleza huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya kwa mazuwaru na raia wa Iraq kwa ujumla.

Balozi wa Uturuki akaonyesha kuridhishwa na ziara hii, nayo ni ziara yake ya kwanza katika mji mtukufu wa Karbala, Ataba tukufu ni sehemu muhimu kutokana na kufungamana na Maimamu wa Ahlulbait (a.s) akasema kuwa: “Nilihisi mazingira mazuri kiroho nilipokua ndani ya haram hii takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), hali kadhalika nimetembelea makumbusho ya Atabatu Abbasiyya, nimeona mali-kale nyingi zenye maana kubwa”.

Akamaliza kwa kusema: “Natoa shukrani nyingi kwa kila anayefanya kazi katika malalo hii, nitarudi kufanya ziara tena wakati wowote nitakao pata nafasi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: