Zaidi ya wanafunzi 30 wa kiafrika wanashiriki katika somo la Quráni ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kituo cha Dirasaat Ifriqiyya chini ya kitengo cha habari na utamaduni, kwa kushirikiana na Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, wameandaa semina ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s) awamu ya pili, kwa ajili ya kufundisha usomaji sahihi wa Quráni tukufu na hukumu za usomaji pamoja na maandishi ya Quráni kwa wanafunzi wa Dini katika mkoa wa Najafu.

Zaidi ya wanafunzi (30) kutoka nchi tofauti za Afrika wanashiriki kwenye semina hiyo, imefanyiwa ndani ya ukumbi wa Imamu Qassim (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, chini ya ukufunzi wa Ustadh Alaau-Dini Alhamiri mwalimu wa hukumu za usomaji wa Quráni na kiongozi wa idara ya usomaji katika Maahadi, inatarajiwa kudumu kwa muda wa miezi miwili mfululizo, yatafundishwa masomo mengi ya hukumu za usomaji wa Quráni.

Kumbuka kuwa tangu kuanzishwa kwa Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imekuwa ikifanya miradi mbalimbali ya Quráni inayo lenga makundi tofauti, miongoni mwa miradi hiyo ni huu wa kufundisha usomaji sahihi wa Quráni kwa wanafunzi wa Dini unaofanywa na tawi la Maahadi katika mkoa wa Najafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: