Chuo kikuu cha Alkafeel kinaadhimisha siku ya kimataifa ya shindikizo la damu

Maoni katika picha
Chuo kikuu Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kimeadhimisha siku ya kimataifa ya shindikizo la damu, kwa kufanya program ya kielimu iliyo andaliwa na tawi la famasia katika kitivo cha famasia, ikiwa ni sehemu ya miradi yake ya kielimu.

Program hiyo imeendeshwa chini ya uongozi wa chuo na kuhudhuriwa na rais wa chuo Dokta Nuris Muhammad Shahidi Dahani, na wasaidizi wake wa taaluma na idara, pamoja na mkuu wa kitivo cha famasia na walimu wa kitivo hicho, bila kuwasahau wanafunzi wa famasia wa hatua ya nne, inalenga kujenga uwelewa kuhusu tatizo la msukumo wa damu, na kutambua kiwango cha kawaida, pamoja na kuijulisha jamii maradhi hayo na visababishi vyake pamoja na njia za kujikinga, na kuangazia ukubwa wa tatizo la maradhi ya msukumo wa damu katika jamii.

Dokta Saad Mashkuur mkuu wa kitivo cha famasia amesema: “Hakika tatizo la shindikizo la damu ni moja ya sababu kubwa ya vifo vya mapema duniani, viashiria vya maradhi hayo vinaweza visionekane wazi, kujikinga na kujitubu kupo mikononi mwetu”.

Akasema: “Maradhi ya shindikizo la damu hupata watu wengi duniani, kutokana na kuwepo kwa tatizo hilo, chuo chetu kimeamua kuendesha program ya kutambulisha maradhi hayo na hatari yake, pamoja na kuhimiza kuchukua tahadhari za kujikinga nayo”.

Naye Dokta Muhammad Daakhil Rikabi mmoja wa wakufunzi wa chuo amesema: “Tumekua tukihimiza wanafunzi na kuwajengea uwelewa wa kujikinga na maradhi hayo kwa ujumla, program hii tunaifanya sambamba na kuadhimisha siku ya shindikizo la damu kimataifa, wanafunzi wamefanya mazowezi ya kutambua dawa zinazo tumika kutibu tatizo la msukumo wa damu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: