Chuo kikuu cha Al-Ameed kinaendesha opresheni ya kuwachanja watumishi wake dhidi ya virusi vya Korona

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed kimewapa chanjo ya Korona watumishi wake, kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala/ kitengo cha afya katika kituo cha Ghadiir.

Chanjo wanayo pewa inatoka shirika la (Pfizer) la Marekani baada ya kuwasiliana na idara ya afya ya mkoa, katika awamu ya kwanza jumla ya watumishi (60) wamepewa chanjo.

Watumishi wengine watapewa siku zijazo, chanjo hiyo inatarajiwa kutolewa kwa watumishi wote pamoja na wanafunzi wa chuo.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Al-Ameed kimesha fanya semina nyingi kuhusu chanjo, pamoja na harakati zingine tangu kugundulika virusi vya Korona hapa Iraq hadi sasa, ikiwa ni sehemu ya ushiriki wake katika kupambana na janga la Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: