Watumishi wa kikosi cha Abbasi wanapuliza dawa katika mji wa Baabil

Maoni katika picha
Watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji wanapuliza dawa katika mkoa wa Baabil, sehemu walizo puliza ni kituo cha polishi cha mkoa wa Baabil/ kitengo cha kuhakiki makosa ya jinai, idara ya kusajili jinai na vyumba vyote pamoja na njia zote.

Kazi hii itaendelea hadi hatari ya virusi itakapoisha, sehemu kubwa ya barabara na makazi ya watu itapulizwa dawa.

Wananchi wameushukuru uongozi wa kikosi cha Abbasi, kwa kazi kubwa wanayofanya ya kupambana na virusi vya Korona kwa ajili ya kulinda afya ya raia.

Tambua kuwa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, kimeshafanya kazi nyingi za kipinaadamu, ikiwa ni pamoja na kupuliza dawa katika mikoa tofauti, na kujenga kituo cha (Yaasin) katika mkoa wa Karbala, kinacho simamia maziko ya watu waliokufa kwa Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: