(Atwaau-Shabaab) lipo katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa katika mji wa Kuut

Maoni katika picha
Jarida la (Atwaau-Shabaab) linalotolewa na kituo cha ubunifu chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, limepata muitikio mkubwa kutoka kwa vijana wanaotembelea maonyesho hayo yanayo fanywa kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi wa chuo kikuu cha Kuut kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Waasit, kutokana na mada za jarida hilo kugusa makundi muhimu katika jamii, pamoja na kutaja changamoto zao na njia za kuzitatua.

Ustadh Haidari Faaiq katibu wa wahariri wa jarida la mtandao wa Alkafeel amesema: “Jarida linaumuhimu mkubwa, ukizingatia umuhimu wa kundi linalo lengwa, kwani ndio umri muhimu katika jamii, linaelekeza fikra zao na kuwaongoza katika mambo yenye manufaaa pamoja na kupambana na changamoto za maisha, na kuwahimiza kuwa wabunifu kwani wao ndio msingi wa jamii, hakika hili ni jarida muhimu linalo andika mambo ya aina tofauti”.

Akaongeza kuwa: “Jarida linamilango tofauti, kuna mlango wa mambo ya kitamaduni, Itikadi, michezo na teknolojia, jambo ambalo limesababisha kuwa jarida la pekee na kuwa karibu zaidi na vijana, mambo haya yamethibitishwa na wasomaji wake”.

Akamaliza kwa kusema: “Jarida hupenda kuhudhuria katika maonyesho kama haya, kwa ajili ya kudumisha ukaribu wake na vijana, na kupata maoni yao na mapendekezo yao, sambamba na kukuza uwelewa kiakili, kiroho na kimaadili kwa vijana”.

Kumbuka kuwa jarida la Atwaau-Shabaab linapokea maoni ya wasomaji na kuwasiliana nao moja kwa moja, kupitia ukurasa wake wa (facebook) au parua bebe zifuatazo: (ataa@alkafeel.net)‎ au (info@alkafeel.net‏).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: