Kituo cha miradi ya Quráni kinaendelea na vikao vya usomaji wa Quráni katika mikoa ya Iraq

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Quráni chini ya Maahadi ya Quráni kinafanya vikao vya mradi wa minara ya nuru katika mikoa ya Iraq, jengo ka Imamu Hassan Almujtaba (a.s) katika mji wa Bagdad limeshuhudia kikao cha usomaji wa Quráni kwa kushirikiana na kamati ya vijana Almuntadhir (a.f).

Kikao hicho kimehudhuriwa na kundi la wasomaji wa Quráni, wakiwemo wasomaji wa Ataba mbili tukufu, bwana Osama Karbalai na msomaji wa Atabatu Abbasiyya bwana Muhammad Ridhwa Salmaan na Hussein Sawiadi, huku neno la ukaribisho likitolewa na Sayyid Ni’matu Mussawi.

Tambua kuwa kituo cha miradi ya Quráni kimesha fanya makumi ya vikao vya usomaji wa Quráni kwenye mikoa tofauti ya Iraq, kwa kushirikiana na taasisi za Quráni kupitia mradi wa minara ya nuru unaolenga kufundisha utamaduni wa kufanyia kazi mafundisho ya Quráni.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni kupitia matawi yake tofauti ni sehemu muhimu ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga kutoa mafunzo ya Quráni na kutengeneza jamii yenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika sekta tofauti za Quráni tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: