Tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu yanayo fanyika katika mji wa Kuut imepata muitikio mkubwa

Maoni katika picha
Tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu linalo shiriki kwenye maonyesho ya kimataifa ya vitabu yanayo fanyika kwa mara ya kwanza katika mji wa Kuut, limepata muitikio mkubwa kutoka kwa watu wanaotembelea maonyesho hayo, kwani linavitabu vinavyogusa hisia za wasomaji kielimu na kitamaduni.

Miongoni mwa vitabu vinavyo vutia watu wengi kwenye tawi hilo ni (Mausua fatwa ya jihadi kifaya ya kujilinda) kilicho zinduliwa siku ya kuadhimisha kumbukumbu ya kutolewa kwa fatwa tukufu, kitabu hicho kinajuzuu (62) halafu kuna chapisho lingine lisemalo: (Almaswabiih: sherehe ya dua zilizo chaguliwa kutoka kwenye Swahifatu-Sajjaadiyya) kimekusanywa kutokana na khutuba za Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi alizotoa kupitia mimbari ya swala ya Ijumaa, ni moja ya kazi ya kituo cha elimu na ubunifu chini ya kitengo cha habari na utamaduni.

Pamoja na vitabu hivyo, kuna kitabu kingine pia kimepata muitikio mkubwa nacho ni (Kufungua pazia kuhusu maana ya Khutuba mbili za Zaharaa (a.s) sherehe na maelezo) kilicho andikwa na Dokta Karim Hussein Naaswihi Alkhalidi, kimeandika kuhusu changamoto za kinafsi na matatizo ya Fatuma aliyosema katika khutuba yake mashuhuri ya kwanza, aidha kuna vitabu vingi vilivyo pata muitikio mkubwa kutoka kwa watu wanaotembelea maonyesho haya, miongoni mwa vitabu vya dini, sekula, utamaduni, watoto na vinginevyo.

Kumbuka kuwa maonyesho haya ni sehemu ya kubadilishana mawazo na kutambua kazi zinazo fanywa na vitengo pamoja na vituo vya tafiti na malengo ya kuanzishwa kwake kupitia vitabu vyao mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: