Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya, inaendelea na usomaji wa Quráni tukufu chini ya mradi wa kuhuisha usomaji wa Quráni majumbani.
Kikao cha usomaji wa Quráni iliyosomwa kwa ajili ya kumrehemu mmoja wa watumishi wa Ahlulbait (a.s) kimepata mahudhurio makubwa ya viongozi wa Dini na siasa, msomaji wa Atabatu Abbasiyya Dokta Rafii Al-Aamiri pia ameshiriki, na msomaji wa Raudhat ya Qassim Sayyid Hassan Dhabhawi pamoja na wasomaji wa mashairi ya Ahlulbait (a.s).
Tambua kuwa Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Baabil imesha fanya visomo vya Quráni sehemu mbalimbali ndani ya mkoa wa Baabil kupitia mradi huu, kwa lengo la kutengeneza kizazi kinacho fanyia kazi mafundisho ya vizito viwili.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu kupitia matawi yake tofauti ni sehemu muhimu ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, inalenga kutoa elimu ya Quráni, na kutengeneza jamii ya wasomi wanaoweza kufanya tafiti za kielimu ndani ya Quráni tukufu.