Semina kuhusu huduma ya uokoaji kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Idara ya Swidiqatu-Zaharaa (a.s) chini ya ofisi ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendesha semina mbalimbali kwa watumishi wake kuhusu utoaji wa huduma ya kwanza (uokozi), kwa kushirikiana na ofisi ya shule za Alkafeel za wasichana.

Kiongozi wa idara hiyo bibi Bushra Kinani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Miongoni mwa malengo ya idara ni kusimamia sekta ya malezi, na kuandaa idadi kubwa ya watoa huduma ya uokozi, kutokana na umuhimu wa jambo hilo, hasa wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, na kuhakikisha mazuwaru wanapata huduma bora za matibabu”.

Akaongeza kuwa: “Semina imefanyiwa ndani ya ukumbi wa kituo cha Swidiqatu-Zaharaa (a.s), kwa muda wa saa nne kila siku, ambapo wanasoma siku sita kwa wiki, chini ya ukufunzi wa wataalamu wa idara ya afya ya Karbala na hospitali ya rufaa Alkafeel, wanafundisha kwa nadhariyya na vitendo, ikiwa ni pamoja na kuonyesha mbinu za msingi katika uokozi, kwa mfano kuokoa mtu aliyejeruhiwa, aliye ungua, aliyevunjika kiungo, aliyezimia, aliyeshindwa kupumua, uokozi wa watoto, mtu mwenye tatizo la moyo na mengineyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: