Wakuu wa vyuo vya kiislamu nchini Iraq wametembelea kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati.

Maoni katika picha
Kamati ya wakuu wa vyuo vya kiislamu chini ya wizara ya elimu ya juu na tafuti za kielimu hapa Iraq, wametembelea kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya vyuo hivyo na kitengo cha kiislamu, sambamba na kuangalia harakati zake katika mambo mbalimbali ya kiitikadi, kifalsafa na kifikra.

Dokta Muhammad Zawin na Sattaar Aáraji wameeleza malengo ya kielimu na nafasi ya kituo katika kuanzisha mfumo wa kifikra katika (kutatua, kuzuwia, kutengua na kujibu) kupitia maeneo tofauti ya (fikra za kiislamu, kimashariki na kimagharibi), kupitia njia tofauti, vitabu, majarida, semina na makongamano.

Dokta Muhammad Jawaad Twarihi rais wa wakuu wa vyuo vya kiislamu na wajumbe aliofuatana nao, wamefurahi sana na kupongeza harakati zinazofanywa na kituo pamoja na machapisho yake ya kimkakati na kielimu, wakaonyesha utayali wao wa kushirikiana na kudumisha mawasiliano na vyuo vyao, sambamba na umuhimu wa kufikisha machapisho ya kituo hiki katika vyuo vingine vinavyo fanana na chuo hiki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: