Mwaka mmoja uliopita: Atabatu Abbasiyya tukufu ilizindua mtambo wa Oksijen katika hospitali ya Hussein mjini Naswiriyya

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo mwaka jana (2020m), Atabatu Abbasiyya tukufu iliipa hospitali ya Hussein (a.s) katika mkoa wa Dhiqaar mitambo miwili ya Oksijen, kusaidia kupunguza tatizo la upungufu wa Oksijen lililokuwepo katika hospitali hiyo.

Huo haukuwa msaada wa kwanza kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, ukurasa wake wa misaada ya kibinaadamu umejaa aina tofauti za misaada, mitambo hiyo ilitolewa baada ya kupokea maombi kutoka kwa madaktari wa hospitali pamoja na wakazi wa mkoa huo, walio lalamikia upungufu wa Oksijen, uliosababisha madhara makubwa wa wagonjwa wanaolazwa huku wengi wao wakiwa na tatizo la maambukizi ya virusi vya Korona.

Baada ya kupokea maombi tulifanya haraka kuwapa mitambo hiyo chini ya usimamizi wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, chini ya kauli mbiu isemayo (tatua tatizo bila kuangalia sababu za tatizo), tuliwapa mitambo miwili ndani ya muda usiozidi saa (12), ikaunganishwa na mtambo mkuu wa hospitali hiyo bila kutokea tatizo lolote, pamoja na kuwepo joto kali na maambukizi ya virusi vya Korona.

Mitambo hiyo inatumia teknolojia ya (psa) inayotumika kusambaza Oksijen kwenye mitungi, kwa ujazo wa mita (36) kwa saa, jambo ambalo limeondoa tatizo la Oksijen kabisa katika hospitali hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: