Mkuu wa uendelezaji wa viwanda ametembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Mkuu wa idara ya kuendeleza viwanda katika wizara ya viwanda na madini ya Iraq bwana Azizi Naadhim Abdu ametembelea viwanda vya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Katika ziara hiyo amefuatana na msaidizi wake wa idara ya biashara kwa lengo la kuangalia uzalishaji wa viwanda hivyo.

Tumeongea na Sayyid Azizi Naadhim Abdu kuhusu ziara hiyo, amesema: “Kutokana na mualiko tuliopewa na Atabatu Abbasiyya kupitia shirika la biashara Alkafeel, tumetembelea miradi muhimu ya viwanda, miongoni mwake ni shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud”.

Akaongeza kuwa: “Tumeangalia uzalishaji wa shirika la Khairul-Juud wa mbolea, vitakasa mikono na barakoa,”. Akafafanua kuwa: “Kisha tukaenda kituo cha uchapaji na usambazaji wa vitabu Darul-Kafeel, mkuu wa kiwanda hicho ameeleza namna wanavyo chapisha aina tofauti za vitabu na madaftari yanayo tumika kujifunzia shuleni”.

Akaendelea kusema: “Tumeona utendaji bora katika miradi ya viwanda, hiyo ni sababu kubwa ya maendeleo ya viwanda vya sasa, ukilinganisha na teknolojia ya viwanda vya zamani”.

Akasisitiza kuwa: “Viwanda vya Atabatu Abbasiyya tukufu vinamchango mkubwa katika kuboresha sekta ya viwanda hapa nchini”.

Mkuu wa maendeleo ya viwanda amesema: “Tunafanya kila tuwezalo katika kusaidia maendeleo ya kiwanda, lakini miradi ya viwanda inayofanywa na Atabatu Abbasiyya imepiga hatua kubwa”.

Akafafanua kuwa: “Msaada wetu umejikita katika kurahisisha uingizaji wa malighafi na punguzo la kodi pamoja na kurahisisha mchakato wa mkopo kwa ajili ya kiwanda”.

Kumbuka kuwa ziara hii ni sehemu ya ratiba ya mawasiliano endelevu ya Atabatu Abbasiyya pamoja na wizara tofauti, kwa lengo la kubadilishana uzowefu na kuleta maendeleo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: