Kituo cha kupiga picha nakala-kale na faharasi kimetoa faharasi ya nakala-kale ya maktaba ya muandishi wa Jawaahir

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha kupiga picha nakala-kale na faharasi chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat katika Atabatu Abbasiyya kimetoa kitabu cha (faharasi ya nakala-kale za maktaba ya muandishi wa Jawaahir), nayo ni miongozi mwa maktaba za kwanza kupigwa picha katika mji wa Najafu, na kuandaliwa faharasi yake kisasa chini ya misingi mipya inayotumika.

Mkuu wa kituo hicho Ustadh Swalahu Siraji ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tunaangazia historia ya kuzaliwa msomi aliyetumia umri wake katika kuandika vitabu, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu tumefanikiwa kuandaa faharasi ya maktaba ya muandishi wa Jawaahir, na kukubaliana na mhakiki Fadhili Ahmadi Ali Majidi Alhilliy kuandaa faharasi ya kielimu, kitengo kimechukua jukumu la kugharamia kazi hiyo, na kuichapisha katika muonekano mpya”.

Akaongeza kuwa: “Faharasi imetambulisha majarida (349) yaliyo andikwa, yakiwa na mada (398) miongoni mwake (25) zikiwa na mada (74), huku mada nane zikiwa zimeandikwa kwa lugha ya kifarisi, hali kadhalika vimetajwa vielelezo vya kihistoria (397)”.

Akaendelea kusema: “Mwishoni mwa kitabu kunamaelezo ya baadhi za sekta, yaliyokusanywa kwenye faharasi (19) kupitia kitabu cha (Maneno katika kusherehesha sheria za kiislamu), jumla kuu ya mada za kitabu hicho ni (417) katika juzuu (368)”.

Kumbuka kuwa kituo cha kupiga picha nakala-kale na faharasi tangu kilipo anzishwa kimechukua jukumu la kupiga picha nakala-kale na kutengeneza faharasi kwa ajili ya kutumiwa na wasomi pamoja na watafiti, tayali kimesha piga picha nyingi za nakala-kale katika miji tofauti ya Iraq na kwenye ulimwengu wa kiislamu.

Kuingia katika mtandao maalum wa kituo tumia moja ya anuani zifuatazo:

Facebook: www.facebook.com/mpualkafeel2019

Toghuti maalum ya kituo: https://alkafeel.net/library/photos/

Kutafuta anuani za nakala-kale: https://dromh.org
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: