Mlango wa pili kwa ukubwa katika Atabatu Abbasiyya tukufu unawekwa Kashi-Karbalai

Maoni katika picha
Watumishi wanaofanya kazi katika mradi wa kukarabati milango ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ndani, wameanza kuweka Kashi-Karbalai katika mlango wa Inamu Hassan (a.s), nayo ni miongoni mwa kazi za mwisho katika mlango huo, baada ya kumaliza kazi nyingi za utangulizi.

Kiongozi wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi inaendelea kwenye mlango huo wa pili kwa ukubwa katika Atabatu Abbasiyya baada ya mlango wa Kibla, unao elekea katika uwanja wa katikati ya haram mbili, chini ya mradi wa uendelezaji wa milango ya malalo takatifu, kwa usanifu bora na muonekano mzuri unao endana na milango mingine”.

Akasema: “Hatua ya kwanza katika ujenzi huo imehusisha kutoa rangi ya zamani na kurekebisha ukuta pamoja na kufunga nyaya za baadhi ya mifumo, hadi kufikia hatua ya kuweka Kashi-Karbalai sehemu ya juu ya mlango, tumeweka nakshi na mapambo maalum, kazi imekamilika kwa kiwango cha asilimia % 80, na bado inaendelea”.

Akamaliza kwa kusema: “Mafundi wa shirika linalofanya kazi hiyo chini ya shirika la ujenzi la Ardhi takatifu, wameweka mkakati wa kukarabati milango yote tisa ya Atabatu Abbasiyya, kwa namna ambayo itaendana na sehemu ilipo kwa nje na ndani”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imekusudia kukarabati milango yote ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), katika mradi wa upanuzi wa haram tukufu ukizingatia kuwa ndio sura ya Ataba takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: