Kituo cha Multaqal-Qamaru kimepokea kundi la vijana kutoka Diyala

Maoni katika picha
Kituo cha Multaqal-Qamaru chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimepokea kundi la vijana (wanaofanya kazi chini ya usimamizi wa muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mkoa wa Diyala).

Mkuu wa kituo Shekh Haarith Dahi amesema: Ugeni huu ni sehemu ya kuwajenga vijana kifikra, kimaarifa na kiakili, na kuwafanya kuwa kigezo chema katika jamii.

Akaongeza kuwa: “Tumepokea kundi hili ambalo imelazimu kuwa na idadi maalum ya vijana (30) kutokana na kuwepo kwa janga la virusi vya Korona, ujio wao ni sehemu ya matunda ya ziara tuliyofanya katika mkoa wa Diyala, tulijadili mambo mengi katika ziara hiyo, ikiwa ni pamoja na kufungua milango ya kupokea makundi ya vijana katika Atabatu Abbasiyya na kuwapa semina, warsha, nadwa zinazo lenga kujenga mwanaadamu bora katika jamii”.

Akafafanua kuwa: “Ratiba yao itachukua siku nne, na itafuata ratiba ya makundi mengine Insha-Allah, tunatarajia kufikia idadi kubwa zaidi ya vijana, ili waweze kuwa na athari katika jamii”.

Akasisitiza kuwa: “Kufanyika kwa ratiba hii kunatokana na maombi ya muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mkoa wa Diyala Mheshimiwa Shekh Abdurazaaq Faraju-Llah, kwa wasimamizi wa ratiba hii na kuwaomba wawape kipaombele vijana wa kiislamu, pamoja na kuishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu na watumishi wake kwa kuwa na program za aina hiyo, za kupokea vijana na kuwafundisha maadili mema”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: