Kuanza kazi ya kuongeza sehemu mpya katika uwanja wa Aljuud

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wameanza kazi ya ujenzi katika eneo lililo ongezwa hivi karibuni kwenye uwanja wa Aljuud, upande wa kushoto wa barabara ya Baabu-Qibla katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ujenzi umeanza baada ya kumaliza kazi ya kubomoa na kuondoa mabaki yote ya majengo yaliyo bomolewa, eneo hilo linamilikiwa na Ataba tukufu, linaukubwa wa mita za mraba (1450).

Hii ni hatua ya tatu ya upanuzi katika uwanja huu wa haram, ipo ndani ya mradi wa upanuzi unaotekelezwa na Ataba tukufu, unaolenga kuongeza sehemu kubwa itakayo saidia kutoa huduma kwa mazuwaru.

Ustadh Hassan Abdulhussein msimamizi mkuu wa ujenzi huo ameuambia mtandano wa Alkafeel kuwa: “Ujenzi umeanza baada ya kuondoa mabaki yote ya majengo yaliyo bomolewa sehemu hiyo, kazi ya kwanza ilikuwa ni kujenga tabaka la chini ambalo ni muhimu sana, hivyo ujenzi umefanywa taratibu na kwa weledi mkubwa ukizingatia kuwa msingi lazima uwe imara, baada ya kumaliza tutaingia hatua nyingine, na ujenzi utafanyika hatua kwa hatua”.

Akaongeza kuwa: “ujenzi umehusisha mfumo wa (umeme – mawasiliano – kamera na maji safi ya kunywa), kila mfumo umeunganishwa na mfumo wa zamani uliokuwepo, chini ya utaratibu maalum ulio andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Kumbuka kuwa ujenzi huu unafanywa ili kupunguza msongamano wa watu ambao hutokea katika eneo hilo, na kuongeza uwezo wa kupokea idadi kubwa zaidi ya mazuwaru, hususan katika ziara zianazo hudhuriwa na mamilioni ya watu ambazo huwa na msongamano mkubwa, unaosababisha usumbufu katika kufanya ziara na wengine kushindwa kuingia ndani ya Ataba takatifu, hii ni moja ya sehemu muhimu kwa watu wanaokuja kutembelea malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: