Mwezi ishirini na tano Dhulqaadah ni siku ya kutandikwa ardhi na kuenea kwa rehema za Mwenyezi Mungu

Maoni katika picha
Ardhi ilitandikwa siku ya mwezi ishirini na tano Dhulqaadah, ni tukio kubwa la uumbaji wa Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu mtukufu anasema: (Na ardhi baada ya hapo akaitandika), Annaaziaat/30, yaani akaitandika na kuifanya kuwa mahali pazuli pakuishi, katika kitabu cha (Muhawalaatu lifahmi asriy lil-Quráni) neno “Dahaaha”maana yake: (akaifanya kama yai) na ndio mtazamo wa kisasa wa wana-anga kuhusu umbo la ardhi..

Neno (dahaa) linamaana ya kutandika, nalo ni neno pekee la kiarabu lenye maana ya kutandika na kutengeneza umbo la duara kwa wakati mmoja, nalo ndio neno bora kwa maana hiyo.

Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu alitandika ardhi kuanzia chini ya Kaaba tukufu, Mwenyezi Mungu alikuwa amesha umba ardhi toka zamani, siku ya mwezi ishirini na tano Dhulqaada akaitandika, mtazamo huu unaungwa mkono na hadithi nyingi, imepokewa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu alitandika ardhi kuanzia chini ya Alkaaba tukufu hadi Mina, kisha akaitandika kuanzia Mina hadi Arafa, kisha Arafa hadi Mina na Mina hadi Alkaaba) tafsiri Nuuru Thaqalaini juzuu ya 5/ ukurasa wa 502.

Hakika sehemu ya kwanza kuumbwa katika ardhi ni pale ilipo Kaaba takatifu, kisha Mwenyezi Mungu akatandika ardhi kuanzia sehemu hiyo, na ndio maana ya maneno ya Mwenyezi Mungu mtukufu yasemayo: (Hakika nyumba ya kwanza kujengwa kwa ajili ya watu ni ile iliyopo Bakkah takatifu).

Siku hii tukufu ni suna kufanya mambo yafuatayo:

  • - Kufunga: kuna riwaya nyingi zinazo sisitiza kufunga siku hiyo, miongoni mwa riwaya hizo ni: Mtume (s.a.w.w) anasema: (Mwenyezi Mungu alishusha rehema katika siku ya mwezi ishirini na tano Dhulqaadah, atakaefunga siku hiyo, ataandikiwa thawabu sawa na aliyefunga miaka sabini).
  • - Dua: ni sunna kusoma dua ifuatayo: (Ewe Mola uliyetandika ardhi, na kutoa mbegu, muondoaji wa matatizo, nakuomba katika siku hii….) hadi mwisho wa dua kama ilivyo andikwa katika kitabu cha Mafaatihu-Jinaani na kwenye vitabu vingine vya dua.
  • - Swala: uswali rakaa mbili wakati wa Dhuha, usome Alhamdu mara moja na washamsi mara tano katika kila rakaa, baada ya salamu useme: (Laahaula walaa Quwata Illa Billahil-Aliyyil-Adhim), kisha usome dua ifuatayo: (Ewe muondoaji wa matatizo ondoa matatizo yangu, ewe mwenye kukubali maombi kubali maombi yangu, ewe mwenye kusikia sauti sikia sauti yangu, nihurumie na unisamehe dhambi zangu na makosa yangu, ewe mwingi wa utukufu na ukarimu).

Katika baadhi ya vitabu vya dua imeandikwa kuwa, kwenda kumzuru Imamu Ridhwa katika siku hiyo ni miongoni mwa ibada kubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: