Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Hindiyya chini ya Atabatu Abbasiyya, imefanya nadwa ya Quráni chini ya anuani isemayo: (Quráni tukufu na msimamo wake kuhusu migogoro), na kuhudhuriwa na kundi la waumini na wadau wa Quráni.
Nadwa imefunguliwa kwa Quráni iliyosomwa na Yusufu Fatalawi, ukafuata ujumbe kutoka kwa kiongozi wa tawi la Hindiyya Sayyid Haamid Marábi, akaelezea miradi ya tawi hilo na lengo la kufanya nadwa hizi zinazo kusudia kutoa elimu ya kitabu kitakatifu.
Kisha mhadhiri wa nadwa hiyo Dokta Muhammad Hussein Abuud ambaye ni mkufunzi wa kitengo cha elimu za kiislamu katika chuo kikuu cha Karbala, akaanza kuwasilisha mada yake, kwa kueleza maana ya migogoro, ambayo imekua ikipotoshwa katika mafundisho ya Dini tukufu ya kiislamu.
Akafafanua baadhi za aya ndani ya Quráni zinazo kemea chuki na migogoro, pamoja na kukataza kila aina ya shari bila kujali chanzo chake, akatoa ushahidi mwingi wa aya na hadithi tukufu, akaashiria tukio la kuuwawa kwa Imamu Hussein (a.s) kuwa ni moja ya kielelezo kikubwa cha migogoro na chuki kubwa aliyokuwa nayo Yazidi na wafuasi wake.
Kumbuka kuwa tawi la Maahadi katika wilaya ya Hindiyya hufanya harakati mbalimbali za Quráni, zikiwemo nadwa za Quráni, Dini na Utamaduni kwa lengo la kujenga utamaduni wa kushikamana na vizito viwili katika jamii.