Idara ya Quráni imetangaza kufanya semina ya (Yanabia-Rahmah lil-yaafiyaat)

Maoni katika picha
Idara ya Quráni chini ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kufanya semina iliyopewa jina la (Yanabia-Rahmah lil-yaafiyaat), awamu ya pili.

Kiongozi wa idara bibi Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi amesema: “Semina itakuwa na masomo mengi, miongoni mwa masomo hayo ni (Fiqhi, Aqida, Kusahihisha usomaji wa Quráni, Hukumu za usomaji, Kazi za mikono, Historia na utamaduni wa familia).

Akaongeza kuwa: “Washiriki wa semina hii wanaokusudiwa ni wale waliozaliwa mwaka (2006 – 2007 – 2008) mwisho wa kujisajili ni tarehe tisa ya mwezi huu”.

Akabainisha kuwa: “Semina itafanywa asubuhi ya (Jimapili, Jumatatu na Jumatano) ya kila wiki, kuanzia tarehe kumi na mbili mwezi wa saba (12/7) hadi tarehe tisa mwezi wa nane (9/8)”.

Akasema kuwa: “Kujiandikisha kushiriki semina hii kunafanyika katika ofisi za idara ya Quráni ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) upande wa wasichana, mshiriki aje na nyaraka zinazohitajika ambazo ni: kitambulisho cha taifa, au kitambulisho chochote pamoja na picha mbili ndogo, afike asubuhi au jioni katika ofisi za idara ya Quráni kwa ajili ya kujaza fomu, tambua kuwa usafiri wa kubeba wanasemina utakuwepo wakati wote wa semina”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: