Mashamba ya barakaatu Ummul-Banina ni moja ya msingi wa uchumi

Maoni katika picha
Mashamba ya barakaatu Ummul-Banina (a.s) yanazalisha mazao ya kimkakati na majani ya wanyama, yanamchango mkubwa katika kuingiza bidhaa bora sokoni.

Tumeongea na rais wa mashamba na bidhaa za wanyama kuhusu mashamba hayo, ambayo yapo chini ya shirika la uzalishaji Alkafeel la Atabatu Abbasiyya tukufu Mhansisi Ali Maz’ali Laaidh amesema: “Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umeweka mikakati mbalimbali ya muda mrefu na muda mfupi, kwa kufanya miradi muhimu, inayo fungamana na uchumi wa taifa, ikiwa ni pamoja na miradi ya kilimo na viwanda”.

Akaongeza kuwa: “Baada ya mafanikio yanayo shuhudiwa katika sekta hiyo, Atabatu Abbasiyya tukufu imeanzisha mashamba ya Barakaatu Ummul-Banina (a.s) kwa aliji ya mazao muhimu ya kimkakati, ikiwa ni pamoja na kilimo cha majani maalum kwa ajili ya chakula cha wanyama”.

Akaendelea kusema: “Shamba linaukubwa wa dunam (620) lipo katika barabara ya (Karbala/Bagdad) katika eneo la Kamaliyya, mazao yanayo limwa ni ngano na shairi pamoja na majani kwa ajili ya chakula cha wanyama wafugwao”.

Akafafanua kuwa: “Hatua ya kwanza ya mradi huu tuliandaa shamba na kuchimba visima, kisha kazi za kilimo zikaanza, baadhi ya mazao hutunzwa kwa msimu ujao na mengine huingizwa sokoni moja kwa moja”

Akasema: “Shamba lina maeneo mawili (2) yaliyojengwa paa ambayo ni sehemu ya kufugia kondoo yenye ukubwa wa (2m3000) kuna kondoo jike (600) na mbuzi, mifigo yote hutegemea kula majani ya shamba hilo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: