Kukamilika kazi ya kutengeneza ufito wa maandishi ya Qur’ani kwenye dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s)

Maoni katika picha
Mafundi wanaofanya kazi katika mradi wa kutengeneza madirisha ya makaburi na milango chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wamekamilisha kazi ya kutengeneza ufito wa maandishi ya Qur’ani utakao kaa juu ya dirisha jipya la malalo ya bibi Zainabu (a.s) linalo endelea kutengenezwa hivi sasa.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo hicho Sayyid Naadhim Ghurabi, akaongeza kuwa: “Utengenezaji wa dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s) unaendelea vizuri kama ulivyo pangwa, sawa iwe katika sehemu za kuwekwa madini au mbao, ufito wa maandishi ya Qur’ani ni moja ya sehemu zilizo kamilika, kilicho baki ni kutiwa dhahabu herufi hizo kazi itakayo fanywa siku zijazo”.

Akafafanua kuwa: “Ufito wa maandishi ya Qur’ani ambao juu yake kuna mstari wa dhahabu, umetengenezwa kwa madini na umeandikwa surat Insaan yote kuanzia (Hal-Ataa alal-insaan…) hadi (Yudkhilu man yashaau fii rahmatihi, wa dhwaalimiina a’adda lahum adhaaban aliimaa),imeandikwa na mwalimu wa hati Dokta Raudhwan Bahiyya kwa hati ya Thuluthu-Murakkab”.

Akabainisha kuwa: “Herufi zinaurefu wa (sm19) huku ufito ukiwa na unaurefu wa mita (16.78) na ujazo wa (ml5), umezunguka dirisha pande zote, aya zimepangwa vizuri, herufi zitawekwa dhahabu halisi na kutiwa mina ya bluu”.

Akamaliza kwa kusema: “Ufito umetengenezwa kwa umaridadi mkubwa sawa na sehemu zingine za dirisha, unaendana vilivyo na sehemu zote za dirisha hilo takatifu, kwani sehemu zote zinaunda kitu kimoja”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: