Majlis ya kuomboleza kifo cha Imamu Jawaad (a.s)

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa husseiniyya tawi la wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu wa tisa Muhammad Aljawaad (a.s), ndani ya sardabu za haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhudhuriwa na mazuwaru pamoja na waombolezaji, kwa kuzingatia kanuni na masharti ya afya ikiwa ni pamoja na umbali kati ya mtu na mtu katika ukaaji.

Makamo kiongozi wa idara hiyo bibi Taghridi Tamimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Majlisi hii inafanywa kwa kushirikiana na ofisi ya Zainabiyyaat katika Atabatu Abbasiyya kutukuza alama za Mwenyezi Mungu kwa kuadhimisha matukio ya Ahlulbait (a.s) na kuomboleza misiba yao, pamoja na mambo yaliyo tokea katika umma wa kiislamu hususan wafuasi wa Ahlulbait katika siku kama hizi, idara inaratiba kamili yakuhuisha matukio ya aina hii, likiwemo hili la kifo cha Imamu Jawaad (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Majlisi itafanywa kwa muda wa siku mbili jioni, baada ya Qur’ani ya ufunguzi hutolewa mawaidha na mmoja wa watumishi wa idara, ambaye huongea kuhusu historia ya Imamu Jawaad (a.s) na mambo muhimu yaliyo mtokea pamoja na dhulma alizo fanyiwa, hadi tukio la kifo chake (a.s), sambamba na kusisitiza umuhimu wa kufuata nyayo zake, na kubeba jukumu la kidini na kibinaadamu”.

Akaendelea kusema: “Kisha husomwa tenzi na mashairi kuhusu msiba huo na huzuni kubwa waliyopata Ahlulbait (a.s) na wafuasi wao, majlisi hufungwa kwa kusoma Duau-Faraji ya Imamu wa zama (a.f) kwa nia ya kukidhi haja na kuondoa mabalaa pamoja na kulilinda taifa la Iraq na raia wake”.

Kumbuka kuwa Imamu Jawaad ni mtoto wa Ali Ridhwa (a.s), ni Imamu wa tisa katika maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s), alizaliwa mwaka wa (195h) akafa mwishoni mwa mwezi wa Dhulqaadah mwaka wa (220h), baada ya kupewa sumu na mke wake Ummul-Fadhil kwa amri ya Mu’utaswimu Abbasi, akafa akiwa bado kijana mwenye umri wa miaka (25) tu, na kipindi cha Uimamu wake kilidumu kwa miaka (17).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: