Maukibu ya watu wa Karbala inayo undwa na vikundi vya mji huo pamoja na wananchi wasiokuwa kwenye vikundi, imeomboleza kifo cha Imamu wa tisa Muhammad Jawaad (a.s) mbele ya malalo ya shangazi yake Fatuma Maasuma mtoto wa Imamu Mussa bun Jafari (a.s) katika mji wa Qum, kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
Rais wa kitengo hicho bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maukibu ya watu wa Karbala imezowea kuhuisha matukio tofauti ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) ndani na nje ya mji wa Karbala, ikiwemo kuomboleza kifo cha Imamu Jawaad (a.s) katika haram ya Maasumah (a.s), Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimeandaa gari na kuwapeleka hadi kwenye mpaga wa Iraq na Iran, na kitengo chetu kimefanya mawasiliano na kuandaa mazingira ya kufanikisha maombolezo hayo”.
Akaongeza kuwa: “Maukibu imempa pole bibi Maasuma (a.s), matembezi ya maukibu yamefanywa kwa vikundi, wakati wa matembezi hayo imeimbwa mimbo na kusomwa mashairi ya kuomboleza yaliyo amsha hisia za huzuni, wakati wa kuingia katika haram takatifu kikafanywa kikao cha kuomboleza na kusomwa tenzi na mashairi mbalimbali, miongoni mwa walio soma tenzi ni Abdul-Amiir Al-Umawi, beti za utenzi wake zimeeleza madhila waliyopata watu wa nyumba ya Mtume (a.s) akiwemo Imamu Jawaad (a.s)”.
Akamaliza kwa kusema: “Mawakibu itakuwa na ratiba ya matembezi ya kuomboleza katika siku hizi, hapa (Qum) na kwenye malalo ya baba yake Imamu Ridhwa (a.s) katika mji wa Mash-had, pamoja na shughuli za uombolezaji tutagawa chakula bure kwa waombolezaji”