Atabatu Abbasiyya imewekwa mapambo meusi kuomboleza msiba wa Imamu Al-Jawaad (a.s)

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imevaa vazi la msiba na kutanda huzuni kutokana na kumbukumbu ya kifo cha Imamu Muhammad bun Ali Al-Jawaad (a.s), aliyefariki mwishoni mwa mwezi wa Dhulqaadah.

Imewekwa vitambaa vilivyo andikwa maneno ya huzuni kama alama ya kuonyesha majonzi ya Ataba tukufu na watumishi wake, na kumpa pole Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), kutokana na msiba huu mkubwa unaoumiza nyoyo za wapenzi na wafuasi wao, hakika ni msiba wa kufiwa na Imamu wa tisa miongoni mwa Maimamu watakatifu walio bashiriwa na Mtume (s.a.w.w).

Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum ya shughuli za uombolezaji wa msiba huu.

Kumbuka kuwa Imamu Muhammad Al-Jawaad mtoto wa Ali Ridhwa (a.s) ni Imamu wa tisa, alizaliwa mwaka wa (195h) na akauwawa kishahidi mwishoni mwa mwezi wa Dhulqaadah mwaka (220h), baada ya kupewa sumu na mke wake Ummulfadhil kwa amri ya Mu’taswimu Abbasi, akafariki akiwa na umri wa miaka (25) na muda wa Uimamu wake ulikuwa ni miaka (17).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: