Jeneza la kuigiza limetembezwa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Asubuhi ya Jumamosi Maukibu ya watu wa Karbala imefanya matembezi kuelekea katika haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kutoa pole kutokana na kifo cha Imamu Muhammad bun Ali Ridhwa Al-Jawaad (a.s).

Matembezi hayo yametanguliwa na jeneza la kuigiza lililobebwa kwa majonzi makubwa, kwenda kumpa pole Mtume wa watu wa nyumbani kwake (a.s) kutokana na msiba huu, kituo cha kwanza ilikuwa ni malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), matembezi hayo yameanzia katika moja ya barabara inayoelekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kuzunguka ndani ya malalo hiyo wakaelekea kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu.

Matembezi hayo yamefanywa kwa vikundi huku wakiimba kaswida na mashairi ya kuomboleza yaliyo taja madhila aliyofanyiwa Imamu (a.s).

Kumbuka kuwa Imamu Muhammad Al-Jawaad mtoto wa Ali Ridhwa (a.s) ni Imamu wa tisa, alizaliwa mwaka wa (195h) na akauwawa kishahidi mwishoni mwa mwezi wa Dhulqaadah mwaka (220h), baada ya kupewa sumu na mke wake Ummulfadhil kwa amri ya Mu’taswimu Abbasi, akafariki akiwa na umri wa miaka (25) na muda wa Uimamu wake ulikuwa ni miaka (17).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: