Majlisi ya kuomboleza kifo cha Baabul-Muraad

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya wahadhiri wa Husseiniyya imeandaa majlisi yakuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s).

Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)chini ya mradi wa Ummul-Banina (a.s), ambao sehemu ya mradi huo ni kuadhimisha mazazi ya Maimamu (a.s) na tarehe ya vifo vyao.

Kiongozi wa idara Shekh Abdu-Swahibu Twaaiy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kuhuisha matukio ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) ni miongoni mwa maadhimisho makubwa, hakika wao ni meli ya kuokoa na ndio waliobeba amana ya uislamu, wanamchango mkubwa sana katika kufafanua mafundisho ya kiislamu”.

Akabainisha kuwa: “Majlisi zinafanywa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa muda wa siku tatu, kutakua na mihadhara miwili kila siku, mmoja asubuhi ambao utahutubiwa na Shekh Hussein Idawi na mwingine jioni utakaohutubiwa na Shekh Ali Shukriy, kila mhadhara unafatiwa na matam”.

Akaongeza kuwa: “Mihadhara imewekwa katika utaratibu huo kwa ajili ya kueleza historia japo kwa ufupi ya Imamu huyu mtukufu, zinazungumzwa mada tofauti ikiwa ni pamoja na nafasi ya Uimamu wake (a.s) na elimu yake, bila kusahau mafundisho yake na hekima zake, na kuhimiza kufanyia kazi mafundisho yake, hasa katika mazingira tuliyonayo na kueleza tukio la kifo chake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: