Idhaa ya Alkafeel ya wanawake inafanya shindano la (Utekelezaji bora)

Maoni katika picha
Idhaa ya Alkafeel sauti ya mwanamke wa kiislamu chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kuanza kwa shindano la (utekelezaji bora), kutokana na uwezo mzuri wa wanawake na kutengeneza fursa za kazi kwa wasichana watakao faulu na kukubali kufanya kazi, aidha shindano hili litasaidia kufungua ukurasa wa habari wa wanawake na kuwasaidia kufikia ndoto zao, na kuamsha jamii kwa ujumla.

Kupitia shindano hili tutapokea wasichana wenye kipaji cha sauti na uwezo wa kuendesha kipindi, watarekodi sauti zao na kuziwasilisha kwenye kamati ya majaji itakayo chagua mwenye (utekelezaji bora) na kumuunganisha na watumishi wa Idhaa kwa ajili ya kuongoza kipindi.

Masharti ya kushiriki:

  • - Kumiliki kadi kutoka kituo cha utamaduni.
  • - Lugha sanifu na matamshi bora ya herufi.
  • - Kuwa na sauti inayoweza kuendesha kipindi cha redio.

Tambua kuwa mtihaji wa mchujo utafanywa katika jengo la Idhaa mkoani Karbala, utaanza Jumatatu ya tarehe (12 Julai) hadi tarehe kumi na tano mwezi huo, kuanzia saa nane na nusu Adhuhuri hadi saa kumi Alasiri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: