Kumbukumbu ya kifo cha Imamu Aljawaad ndani ya ukumbi wa chuo kikuu cha Alkafeel

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s), kwa kufanya majlisi ndani ya ukumbi wa kitivo cha uhandisi.

Majlisi imehudhuriwa na rais wa chuo Dokta Nuris Dahani na wasaidizi wake, pamoja na wakuu wa vitivo vingine bila kusahau wanafunzi na wafanyakazi.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyofuatiwa na mhadhara kutoka kwa Shekh Abdallah Dujaili aliye ongea kuhusu maisha ya Imamu Aljawaad (a.s) na madhila aliyopata kutoka kwa watawala wa zama zake pamoja na subira aliyofanya, na namna alivyo fikisha ujumbe na mafundisho ya baba zake na babu yake Mtume (s.a.w.w) kwa umma, aidha akaongea kuhusu elimu ya Imamu na miujiza yake, akahitimisha kwa kueleza tukio la kifo chake (a.s) linalo umiza na kufanana na kifo cha babu yake Imamu Hussein (a.s), kama kiu kali aliyopata baada ya kula sumu, pamoja na muili wake kuachwa juu ya nyumba yake ukipigwa na jua kwa muda wa siku tatu.

Kumbuka kuwa Imamu Jawaad ni mtoto wa Ali Ridhwa (a.s), ni Imamu wa tisa katika maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s), alizaliwa mwaka wa (195h) akafa mwishoni mwa mwezi wa Dhulqaadah mwaka wa (220h), baada ya kupewa sumu na mke wake Ummul-Fadhil kwa amri ya Mu’utaswimu Abbasi, akafa akiwa bado kijana mwenye umri wa miaka (25) tu, na kipindi cha Uimamu wake kilidumu kwa miaka (17).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: