Mwezi mosi Dhulhijjah kukutana bahari mbili na nuru kwa nuru

Maoni katika picha
Imepokewa kuwa siku ya mwezi mosi Dhulhijjah mwaka wa (2h), siku kama ya leo, Imamu Ali alimuoa Fatuma Zaharaa (a.s), ikaitwa ndoa ya nuru mbili, tukio hilo linapewa umuhimu mkubwa kwa sababu hao ni watu watukufu na bora zaidi baada ya Mtume (s.a.w.w), imepokewa kutoka kwa Khabaab bun Arti anasema: Mwenyezi Mungu mtukufu alimuambia Jibrilu: Ozesha nuru na nuru, walii alikua ni Allah, mposaji Jibrilu, mualikaji Mikaeli, mtangazaji Israfiil, muandaaji Izraeli, mashahidi malaika wa mbinguni na ardhini, kisha Mwenyezi Mungu akauambia mti wa Toba utoe ulicho nacho, ukatoa duru nyeupe, yaquti nyekundu, zabrajad (kito) cha kijani na lulu, ulipo fika usiku wa ndoa Mtume (s.a.w.w) akaja na punda, akamuambia Fatuma apande, akamuamrisha Salman amuongoze na yeye akawa anamuendesha, wakiwa njiani Mtume akasikia sauti, mara akamuona Jibrilu akiwa na malaika elfu sabini, Mtume (s.a.w.w) akamuuliza mmekuja kufanya nini ardhini? Wakasema: tumekuja kumshindikiza Fatuma kwa Ali bun Abu Twalib, akapiga takbira na Mtume akapiga takbira, malaika wakapiga takpira na Mtume (s.a.w.w) akapiga takbira, zikapigwa takbira kwa wingi katika usiku huo.

Matunda ya ndoa hiyo yakawa ni kupatokana kwa watoto watano, ambao ni Maimamu wawili Hassan Almujtaba na bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s), na mabinti wawili ambao ni Zainabu Alkubra na Ummukulthum (a.s), walizaliwa wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w) ndani ya muda wa miaka tisa, na mtoto wa mwisho alikua ni Muhsin (a.s) ambaye mimba yake ilitoka pale mama yake alipo kandamizwa baina ya ukuta na mlango.

Imepokewa katika hadithi liyopo kwenye kitabu cha Kashfu Ghummah kuwa, maswahaba wengi walienda kumposa Fatuma Zaharaa (a.s) lakini Mtume (s.a.w.w) aliwarudisha, alipoenda kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s) uso wake ulichangamka na akafurahi sana, akasema: (Hakuna mtu anayemfaa Fatuma zaidi ya Ali).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: