Harakati za kuomboleza na kutoa huduma za maukibu za watu wa Karbala katika malalo ya Imamu Ridhwa (a.s)

Maoni katika picha
Maukibu ya watu wa Karbala inatoa pole kwa Imamu Ridhwa (a.s) kwenye malalo yake takatifu katika mji wa Mash-had kufuatia kifo cha mwanae Imamu Muhammad Aljawaad (a.s), katika harakati za kuomboleza na kutoa huduma kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Rais wa kitengo hicho bwana Riyadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maukibu ya watu wa Karbala imeomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad mbele ya kaburi la baba yake Imamu Ridhwa (a.s) katika mji mtukufu wa Mash-had, wamefanya mambo mawili.

Kwanza: Wameomboleza na kugawa chakula kwa mazuwaru na waombolezaji.

Pili: Wamefanya majlisi za kuomboleza ndani ya Husseiniyya ya Karbalaiyya iliyopo katika mji wa Mash-had, mzungumzaji alikuwa ni Sayyid Ali Hadaad, akifuatiwa na matam iliyosomwa na Abdul-Amiir Umawiy”.

Akaongeza kuwa: “Hali kadhalika kulikua na matembezi ya uombolezaji ya watu wa Karbala, yaliyoanzia katika moja ya barabara zinazo elekea kwenye haram tukufu, huku wakiwa wamebeba bendera zinazo ashiria huzuni, wakatembea hadi katika haram tukufu wakiwa wanaimba kaswida za kuomboleza kifo cha Imamu wao mtakatifu”.

Kumbuka kuwa Imamu Muhammad Al-Jawaad mtoto wa Ali Ridhwa (a.s) ni Imamu wa tisa, alizaliwa mwaka (195h) na akauwawa kishahidi mwishoni mwa mwezi wa Dhulqaadah mwaka (220h), baada ya kupewa sumu na mke wake Ummulfadhil kwa amri ya Mu’taswimu Abbasi, akafariki akiwa na umri wa miaka (25) na muda wa Uimamu wake ulikuwa ni miaka (17).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: