Watalam wa Alkafeel wa kitengo cha huduma ya kwanza chini ya kitengo cha uboreshaji na maendeleo katika Ataba tukufu wanatoa mafunzo maalum ya utoaji wa huduma ya kwanza, kwa kundi la wanaskaut wa Alkafeel, kwa lengo la kukuza uwezo wa kutoa huduma za kitabibu, na kuwafanya kuwa tayali zaidi.
Kiongozi wa jumuiya hiyo chini ya idara ya watoto na makuzi katika kitengo cha habari cha Atabatu Abbasiyya Ustadh Ali Abduzaid ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hii ni moja ya semina ambazo wanashiriki watoa huduma wa kujitolea, jumla ya watu (75) wameshiriki ambao watasaidia kutoa huduma za matibabu katika mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Akaongeza kuwa: “Ratiba iliyo andaliwa inavipengele vingi, kunamafunzo ya nadhariyya na vitendo, ikiwa ni pamoja na kuhudumia watu wenye matatizo ya moyo na mengineyo”.
Akasema: “Mafunzo yatadumu kwa muda wa siku mbili, saa (12) kwa siku zilizo gawanywa katika nyakati tatu, kila wakati wanafundishwa kwa nadhariyya na vitendo, siku ya mwisho kutakua na mtihani wa kuhitimisha mafunzo”.
Kumbuka kuwa kikosi cha uokozi cha jumuiya ya Alkafeel, kilishiriki kutoa huduma za matibabu katika ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, na walifanikiwa kuokoa watu wengi.